top of page

Moving with the "Freedom" rhythm

Njooni watunzi wote!

Hii ni nafasi yako kuleta “furaha kwa ulimwengu” kwa kutumia vipaji na karama zako za utunzi.

Anza kwa kujikumbusha hisia unayokuwa nayo unapoimba nyimbo za krisimasi. Unaweza kufikiri Kirisimasi ingekuwaje bila nyimbo zile?

Sasa tafakari juu ya matukio muhimu ya kibibiria ambayo kwa marachache au hatuyaimbii kabisa. Maranyingi watu wengi wanaimba kuhusu msalaba, na kidogo kuhusu Ufufuo, je mbona katika maabudu yetu, kunakosekana hisia na mtazamo sahihi kuhusiana na matendo mengi na makubwa ya Mungu? Wacha tufanye ibada halisi.

●      Tuvute umakini wa waabuduo juu ya manukato ya nyumba ya bethania yalivyokuwa pindi Mariamu anampaka Yesu mafuta. 

●      Tufanye masiko ya watu na macho yao kuitazama siku ya pentekoste kule Yelusalemu

●      Katika nyimbo zetu tupake rangi safi picha nzuri za Eden na za Yesu kurudi.

Nyakati hizi saba za shindano la mwaka nzima la SYNC zinaita kwa kulia watunzi wa nyimbo:

Screen Shot 2019-12-09 at 11.37.09 AM.pn
Honor label.jpg

Vipi, hukuzoea utunzi kama huo?

Usijali, wala usikate tamaa. Hakuna watu wengi wanaotunga nyimbo aina hizi. Ndio sababu ya kuitisha shindano—kwa kutafuta watu wanaotunga namna hii tayari, kutangaza kazi yao, na kushawishi wengi wengene ili kujiunga nao kwa kutunga nyimbo aina hizi.  

 

Tunataka Mungu atukuzwe mwaka nzima, si nyakati za Krismasi tu. Zaburi 145.6 inasema, “Watu watatangaza ukuu wa matendo yako ya ajabu, nami nitatangaza ukuu wako.”(BHN) Wimbo wako inaweza kuweka matendo haya kwenye ulimi wa watu. Inaweza kuwa namna moja Mungu anahitimisha ahadi ile. 

 

Wimbo wako inatakiwa kugusa watu kupitia maana ya tukio muhimu la biblia kwa namna ambavyo Nyimbo za Krismasi zinagusa watu kupitia maana ya kuzaliwa Yesu au nyimbo za kuabudu zinagusa watu kupitia maana ya msalaba. Si lazima kwa sauti ya wimbo wako kufanana na Nyimbo za Krismasi ama kwa mfano tenzi za rohoni. Uchague mtindo wowote unaoleta furaha tele kwa wale wanaokuzunguka, iwepo namna fulani kuimba pamoja, kuitikia, n.k. 

 

Ukihisi hata kidogo kwamba Mungu anataka ujaribu aina hii ya utunzi, au tayari una wimbo unaofaa tunachotafuta, karibu sana katika Shindano la Furaha kwa Ulimwengu.

 

Maelekezo kwa Kitengo Kimataifa (kisipo Kiingereza)

Maelekezo kwa Kiingereza juu ya shindano

bottom of page