top of page
Prizes
Eligibility
Purpose
How to enter
Criteria

Tarehe za awamu za shindano (lini nyimbo zitaingizwa)

Kusudi

Masharti ya kushinda

Tuzo

Kustahiki

Jinsi kuingia

Fomu ya kuingiza wimbo

 

AWAMU ZA SHINDANO KUANZIA MWEZI WA TANO 2022 HADI MWEZI WA TANO 2023

Kusanya wimbo wako katika awamu husika ya shindano. Inategemea matendo ya ajabu ya Mungu (matukio/hatua muhimu) ambazo unazingatia. Tazama oroja inayofuata chini;

Awamu A: Nguvu. Tar. 26 Mwezi wa Tano hadi Tar. 6 Mwezi wa Nane, mwaka 2022

 • Tukio Muhimu namba 8: Yesu kugeuka sura. Injili ya Marko 9.1-13. Hakikisho kwenye siri ya nguvu ya Mbingu

 • Tukio Muhimu 14: Upaaji. Matendo ya Mtume 2.21-36. Mfalme kushika mamlaka kwenye kiti chake cha enzi mbinguni

 • Tukio Muhimu 15: Pentecoste. Matendo ya Mtume 2.1-12. Mfalme anaweka Roho wake katika wafuasi wake kuwawezesha nguvu

 

Awamu B: Rehema Tar. 7 Mwezi wa Nane hadi Tar. 6 Mwezi wa Kumi

 • Tukio Muhimu namba 12: Yesu Mkuhani Mkuu wetu. Waebrenia 9.1-15. Sadaka ya mwisho kwa dhambi kwenye mdhabahu mbinguni

 

Awamu C: Ustahimilivu. Tar. 7 Mwezi wa Kumi hadi Tar. 20 Mwezi wa Kumi na Moja, mwaka 2022

 • Tukio Muhimu namba 9: Upako. Injili ya Yohane 12.1-7. Yesu kupakwa mafuta kama Masihi (Aliyepakwa Mafuta)

 • Tukio Muhimu namba 16: Kubeba msalaba ya Yesu. Injili ya Marko 15.15-21 Wafuasi wa Mfalme wanastahimili mateso kwa imani.

 

Awamu D: Maono. Tar. 21 Mwezi wa Kumi na Moja hadi Tar. 31 Mwezi Kumi na Mbili, mwaka 2022

 • Tukio Muhimu namba 6: Bethlehemu. Injili ya Luka 2.1-20. Mtoto anazaliwa kuwa Mfalme

 • Tukio Muhimu namba 17: Kumuita Yesu kurudi. Ufunuo 22.6-21. Wafuasi wa Mfalme wanamtazamia kurudi

 • Tukio Muhimu namba 18: Ulimwengu upya. Ufunuo 11.15-19. Mfalme anarudi kutawala kwa utukufu

 

Awamu E: Uhai. Tar. 1 Mwezi wa Kwanza hadi Tar. 21 Mwezi wa Pili, mwaka 2023

 • Tukio Muhimu namba 1: Uumbaji. Mwanzo 1.1-31. Uumbaji wa ulimwengu na ubinadamu 

 • Tukio Muhimu namba 2: Mnara Babeli. Mwanzo 11.1-9. Maisha yanasambaratika kwa viwango vyote

 

Awamu F: Mizizi. Tar. 22 Mwezi wa Pili hadi Tar. 1 Mwezi wa Nne, mwaka 2023

 • Tukio Muhimu namba 3: Abrahamu. Mwanzo 22.1-18. Ahadi ya kuubariki ulimwengu kupitia uzao wa Abrahamu

 

Awamu G: Uhuru. Tar. 2 Mwezi wa Nne hadi Tar. 17 Mwezi wa Tano, mwaka 2023

 • Tukio Muhimu namba 4: Mapigo na Bahari ya Shamu. Kutoka sura 7-15, hasa 12.1-13. Uokoaji wa Israeli kutoka utumwa katika Misiri

 • Tukio Muhimu namba 5: Nyika. Kumbukumbu la Sheria 29.1-15. Mungu anawavusha watu wake jangwani kuwafikisha Nchi ya Ahadi

 • Tukio Muhimu namba 7: Nazereti (Nyakati mpya). Injili ya Luka 4.14-21. Yesu kutangaza Uhuru

 • Tukio Muhimu namba 10: Jumapili ya Mitende. Mathayo 21.1-16. Kumuinua Mfalme wa Nyakati mpya ya Uhuru.

 • Tukio Muhimu namba 11: Msalaba. Warumi 6.6-10. Yesu anavunja mshiko wa dhambi

 • Tukio Muhimu namba 13: Ufufuo. Injili ya Yohane 20.1-20. Mfalme anashinda mauti kuendelea kuongoza kampeni yake ya uhuru

 

FAQs

Maswali huulizwa?

Iko wapi orodha ya hatua muhimu kwa mpangilio kutoka 1 hadi 18?

KUSUDI

Kutia furaha duniani kwa nyimbo mpya zenye msingi wa “matendo ya majabu” au “matukio muhimu” katika Biblia

MASHARTI TATU YA KUSHINDA

1. Wafurahishe wasikilizaji wako kwa maana na hisia ya moja ya “matendo ya majabu” 18 

Nyimbo za Krismasi zinafurahisha watu kuhusu tendo la ajabu la Mungu (kuzaliwa Yesu) kwa namna nyingi, kwa mfano:

 • Wimbo unaoitwa "Away in a Manger" wenye maana "Mbali kwenye hori” unatupatia picha nzuri ya tukio. Unatupeleka huko.

 • Wimbo unaoitwa "Joy to the world" wenye maana "Furaha kwa ulimwengu" una mstari mmoja tu kuhusu tukio unaosema "The Lord is come" ikimaanisha "Bwana amekuja". Mengine yanayobaki yanazungumzia maana ya tukio na jinsi tunavyoitikia.

 • Wimbo unaoitwa “Hark, the Herald Angels Sing” wenye maana “Sauti kuu, wimbo wa malaika mtangazaji” inasuka pamoja picha ya tukio na maana yake.

 • Wimbo unaoitwa “The Little Drummer Boy” wenye maana “kijana mdogo mpiga ngoma”    huvumbua muhusika ili kuwasilisha baadhi ya maana.

 

2. Kuwa rahisi na furaha kwa kundi kubwa kuimba, kama nyimbo za krismasi (mifano kwenye kipengele cha kwanza)

SIO LAZIMA wimbo wako usikike kama nyimbo za Krismasi, lakini ni LAZIMA uwe rahisi kwa watu wa kawaida (wasio wataalamu) kuimba kwa njia ya kutoka moyoni (kwa hisia). Wimbo unaweza kutungwa kwa kufuata mtindo wowote wa muziki wa kitamaduni au aina yoyote ya uimbaji wa kikundi ikijumuisha mwimbaji pekee au kikundi kinachoimba mistari na kundi jingine kuitikia kwenye kiitikio au seti ya misemo.

Wimbo wako hauwezi kushinda shindano kama utakuwa mgumu sana. Kwa mfano, wimbo wa mtunzi Handel unaoitwa "Hallelujah Chorus" usingeweza kushinda.

 

3. Songesha wasikilizaji wako kuitikia inavyofaa kulingana na tukio muhimu unalolilenga

 • Kwa mfano, wimbo unaoitwa “O Come Let Us Adore Him” unatuita kusherekea na kuabudu.

 • Mfano mwingine ni wimbo unaoitwa “O Holy Night” wenye maana “Ee usiku mtakatifu”  ambao unatutia nguvu kutenda kwa kutuambia kuhusu utawala wa Masihi: “Na kwa jina lake udhalimu wote utakoma.”

TUZO

Zawadi saba za dola za kimarekani 400 katika kitengo cha kimataifa (bila kujumuisha Kiingereza). Shindano lina awamu saba. Zawadi moja kuu ya dola za kimarekani 400 itatolewa kwa wimbo bora katika kila awamu. Haya yatatangazwa mwaka mzima, takriban mwezi moja baada ya kumalizika kwa kila awamu. 

Kutajwa kwa heshima: waamuzi wataamua nyimbo ngapi zinastahili “kutajwa kwa heshima.” Nyimbo hizi zitaangaziwa kwenye tovuti www/SYNCx.org kama nyimbo zilizoshinda zawadi, zenye maelezo na picha ya watunzi wao pamoja na hadithi nyuma ya kila wimbo.

KUSTAHIKI

 

Watunzi wanaweza kushirikishana. 

 

Nyimbo zinaweza kuwa mpya kabisa au zilishachapishwa awali. 

Hakimiliki. Utabaki kumiliki haki ya wimbo wako, lakini lazima uturuhusu kuchapisha maneno kwenye tovuti SYNCx.org. Ikiwa wimbo wako unakiuka hakimiliki, utatolewa kwenye shindano.

Watunzi mahiri na wataalamu wa nyimbo wanastahiki kushindana. Tunatarajia kwamba wengi wanaoingia watakuwa watunzi mahiri, na hawa ni wale tunaotaka kuwatia moyo kupitia shindano. 

Waajiriwa wa SYNCx.org, majaji, pamoja na jamaa zao hawastahiki. 

JINSI KUINGIA  

 • Angalia kujua shindano lipo kwenye awamu gani na ni “matendo ya ajabu” (matukio muhimu) yapi yamejumuishwa katika awamu husika. Awamu moja inaweza kuwa na tukio moja au zaidi, hata tano. Wimbo wako unatakiwa kuzingatia tendo au tukio moja tu, si matendo au matukio yote kwenye awamu.

 • Elekea kwenye tovuti www.SYNCx.org na utafute ukurasa wa “Wazo Kubwa” unaoelezea awamu husika. Kwa mfano, hapa kuna ukurasa wa Wazo Kubwa kwa awamu ya Nguvu inayoanza tar. 26 Mwezi wa Tano hadi tar. 6 Mwezi wa Nane. Soma kurasa wa awamu unayotaka (kwa dakika 3) ili kuona kama Mungu anakupa mawazo yoyote ya wimbo mpya. Pia fikiria nyimbo ambazo tayari umeandika au ulizoandika kiasi ambazo zinaweza kubadilishwa ili zitoshee.

 • Tunga wimbo wako, au chagua wimbo mmoja uliotunga tayari. Angalia sehemu “Masharti matatu ya Kushinda” 

 • Wasikilizishe wimbo wako watu unaowafahamu. Wanapoimba ukague wanafurahia kiasi gani kuimba wimbo wako. Ukaguzi wako huo unaweza kukuambia kama wimbo upo tayari kuwekwa kwenye mfumo wa YouTube.

 • Chapisha wimbo wako kwenye YouTube kwa mfumo wa maneno, yaani ile lyric video. Hivi ndivyo kikundi kinaweza kutazama na kuimba pamoja. Tumia mandhari nyuma iliyo wazi au mchoro rahisi ambao haubaadiliki. Hili ni shindano la utunzi wa nyimbo, si shindano la kutengenza video za muziki.

 • Jiunge na kundi linaloitwa “Joy to the World 2022” kwenye Facebook. (Ikiwa unakwepa Facebook kwa kusudi, tuandikie rasmi kwa maelekezo tofauti.

 • Chapisha Fomu yako ya kuingia kwenye kikundi cha Facebook wakati wowote katika awamu inayofaa. Msimamizi wa kikundi atakujulisha kwamba wamepokea ingizo lako[fomu yako].

 • Ukiwasilisha fomu/wimbo wako mapema vya kutosha wakati wa awamu, unaweza kupata maoni fulani katika kikundi cha Facebook kutoka kwa mkurugenzi wa shindano. Unaruhusiwa kurekebisha wimbo na Fomu yako wakati wowote hadi siku ya mwisho ya awamu ya shindano ambayo wimbo wako unatoshea.  Kumbuka: Mkurugenzi ni mmoja wa majaji; majaji wengine hawapo kwenye kundi la Facebook.

 

Maswali huulizwa - FAQs 

Kwanini zilichaguliwa tarehe hizi?

 

Tarehe hizi zimechaguliwa kulingana na sikukuu. Kwa mfano awamu ya Nguvu ya shindano (au “Awamu Nguvu”) inaanza kwenye Siku ya Upaaji wa Yesu, siku ambayo Yesu alipaa kwenda mbinguni kushika mamlaka kwenye kiti chake cha enzi. Awamu ya Rehema inaendelea hadi juu yake kwenye Siku ya Upatanisho (Yom Kippur), ambayo mwaka huu ni tar. 6 Mwezi wa Kumi.

 

Katika mzunguko wa kila mwaka wa “misimu” ya SYNC, baadhi ya siku kuu zina maana zao za kimapokeo na zingine zina maana tofauti ili kuzalisha mfumo moja unaolinganisha mwaka wa kalenda na hadithi ya Biblia. Inaanza na Mwanzo 1 (uumbaji) kwenye tar. 1 Mwezi wa Kwanza na kumaliza na Ufunuo 22 (Kurudi kwa Kristo) kwenye tar. 31 Mwezi wa Kumi na Mbili.

Matukio Muhimu katika orodha yao 1-18 inakuwaje?

Phases
Dates
Milestones

Matukio Muhimu 18 katika hadithi ya kibiblia ya dunia, kuorodheshwa kihistoria

Matukio saba makuu ya muhimu = 1, 3, 12, 13, 15, 16, 18

Tukio Muhimu namba 1: Uumbaji Mwanzo 1.1-31 (mandhari ya UHAI)

Uumbaji wa ulimwengu na ubinadamu

Tukio Muhimu namba 2: Mnara ya Babeli Mwanzo 11.1-9 (mandhari ya UHAI)

Maisha yanasambaratika katika viwango vyote

Tukio Muhimu namba 3: Abrahamu Mwanzo 22.1-18 (mandhari ya MIZIZI)

Ahadi ya kubariki ulimwengu kupitia wazao wa Abrahamu

Tukio Muhimu namba 4: Mapigo na Bahari ya Shamu Kutoka sura 7-17, hasa 12.1-13 (mandhari ya UHURU)

Uokoaji wa Israeli kutoka utumishi katika Misiri

Tukio Muhimu namba 5: Nyika Kumbukumbu la Sheria 29.1-15 (mandhari ya UHURU)

Mungu anawavusha watu wake jangwani kuwafikisha Nchi ya Ahadi

Tukio Muhimu namba 6: Bethlehemu Injili ya Luka 2.1-20. (mandhari ya MAONO)

Mtoto anazaliwa kuwa Mfalme

Tukio Muhimu namba 7: Nazereti (nyakati mpya) Injili ya Luka 4.14-21 (mandhari ya UHURU)

Yesu kutangaza Uhuru

Tukio Muhimu namba 8: Yesu kugeuka sura Injili ya Marko 9.1-13 (Mandhari ya NGUVU)

Hakikisho kwenye siri ya nguvu ya mbingu

Tukio Muhimu namba 9: Upako Injili ya Yohane 12.1-7 (mandhari ya USTAHIMILIVU)

Yesu kupakwa mafuta kama Masihi (Aliyepakwa Mafuta)

Tukio Muhimu namba 10: Jumapili ya Mitende Mathayo 21.1-16 (mandhari ya UHURU)

Kumuinua Mfalme wa Nyakati mpya ya Uhuru

Tukio Muhimu namba 11: Msalaba Warumi 6.6-10. (mandhari ya UHURU)

Yesu anavunja mshiko wa dhambi

Tukio Muhimu namba 12: Yesu kama kuhani wetu Mkuu Waebrenia 9.1-15 (mandhari ya REHEMA)

Dhabihu ya mwisho ya dhambi kwenye madhabahu ya mbinguni

Tukio Muhimu namba 13: Ufufuo Injili ya Yohane 20.1-20 (mandhari ya UHURU)

Mfalme anashinda mauti kuendelea kuongoza kampeni yake ya uhuru

Tukio Muhimu namba 14: Upaaji Matendo ya Mtume 2.21-36 (mandhari ya NGUVU)

Mfalme kushika mamlaka kwenye kiti chake cha enzi mbinguni

Tukio Muhimu namba 15: Pentekoste Matendo ya Mtume 2.1-12 (mandhari  ya NGUVU)

Mfalme anaweka Roho yake kwa wafuasi wake kuwawezesha nguvu

Tukio Muhimu namba 16: Kubeba msalaba ya Yesu Injili ya Marko 15.15-21 (mandhari ya USTAHIMILIVU)

Wafuasi wa Mfalme wanastahimili mateso kwa imani

Tukio Muhimu namba 17: Kumuita Yesu kurudi Ufunuo 22.6-21. (mandhari ya MAONO)

Wafuasi wa Mfalme wanatazamia kurudi kwake

Tukio Muhimu namba 18: Ulimwengu upya Ufunuo 11.15-19 (mandhari ya MAONO)

Mfalme anarudi kutawala kwa utukufu

Entry form
bottom of page